Saturday, February 27, 2016

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi MUBONDO alitembelea Chuo cha kilimo, mifugo na uvuvi TUMBI Tabora

Mkuu wa Chuo Cha Kilimo, Mifugo na Uvuvi MUBONDO kilichopo mkoani Kigoma Ndugu Hanif Nzully wakijadiliana jambo na Mkuu wa chuo cha Kilimo Mifugo na Uvuvi Tumbi Ndugu Sydney Kasele, pamoja na wakufunzi wengine, wakati wa zoezi la uvunaji wa Tumbaku likiendelea katika moja ya mashamba ya chuo (Pichani kushoto). Pichani kulia Ndugu Sydney Kasele akimkaribisha Ndugu Hanif Nzully katika zoezi la kuhakiki na kuidhinisha matokeo ya astashahada na stashahada ya kilimo na mifugo 2015/2016, muhula wa kwanza wa masomo.