Tuesday, June 4, 2019

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAOMBI YA UDAHILI KWA WAOMBAJI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2019/2020


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo katika Vyuo ambavyo si Vyuo Vikuu ama Vyuo Vikuu Vishiriki nchini. Jukumu mojawapo la Baraza, ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vya Ufundi nchini yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Baraza linapenda kuufahamisha umma kuwa Udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote isipokuwa Ualimu umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 28 Mei, 2019 na utaendelea hadi Tarehe 2 Septemba, 2019 kwa Vyuo vyote vinavyotoa mafunzo katika ngazi hizo. Learn More