Tuesday, June 4, 2019

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAOMBI YA UDAHILI KWA WAOMBAJI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2019/2020


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo katika Vyuo ambavyo si Vyuo Vikuu ama Vyuo Vikuu Vishiriki nchini. Jukumu mojawapo la Baraza, ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vya Ufundi nchini yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Baraza linapenda kuufahamisha umma kuwa Udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote isipokuwa Ualimu umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 28 Mei, 2019 na utaendelea hadi Tarehe 2 Septemba, 2019 kwa Vyuo vyote vinavyotoa mafunzo katika ngazi hizo. Learn More

APPLICATION FORM AND LIST OF INSTITUTES 2019-2020

Application form for Admission into Diploma and Certificate Programmes for the Academic Year 2019/2020.

Download Application form 2019/2020
Download list of Institutes



Tuesday, March 26, 2019

MSIMU WA MAVUNO: Uvunaji wa mahindi ukiendelea katika moja ya shamba la chuo

Zao la mahindi: Mbali na umaarufu wa mkoa wa Tabora katika zao la Tumbaku, Chuo cha kilimo Tumbi kinajihusisha pia na utoaji elimu ya zao la mahindi ikiwa ni sehemu ya masomo kwa wanafunzi. Pichani ni matokeo ya mafunzo kwa nadharia katika uzalishaji wa mahindi na picha zimechukuliwa ikiwa ni kipindi cha mavuno.

Monday, March 25, 2019

MAHINDI: KILIMO CHA ZAO LA BIASHARA





Moja ya mazao ambayo katika chuo mati tumbi wanazalisaha ni pamoja zao la biashara ni mahindi katika mkoa wa tabora tumezalisha idadi kubwa ya mahindi kumeweza kutumia aina ya mbegu ya dk 90-89 ambayo inachukua siku 100 kwa ajili ya kuvunwa.