Wednesday, June 28, 2017

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA STASHAHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za usajili na ithibati, mitaala na upimaji ili tuzo zitolewazo na vyuo/taasisi ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa. Kifungu cha 5 (1) (e) na (f) cha Sheria hii kinaipa mamlaka NACTE, kuanzisha tuzo mbalimbali zinazotolewa na kuhakikisha kuwa ubora wa elimu na mafunzo ya kada ya kati yatolewayo na taasisi mbalimbali yanazingatia ubora unaokusudiwa. Aidha, Kifungu cha 11, kinalitaka Baraza kuhakikisha kuwa Tuzo zitolewazo na vyuo na taasisi zote zinazoendesha mafunzo ya kada ya kati zinatambuliwa na mamlaka husika. Katika muktadha huu, kila chuo/taasisi inayotoa elimu ya ufundi inatakiwa kuwasilisha Baraza matokeo ya mitihani kila mwisho wa semista. Read More