Serikali imesambaza mahindi katika baadhi ya Halmashauri kwa bei nafuu lengo likiwa ni kupunguza bei ya mahindi ambayo wafanyabiashara walikuwa wanayauza kwa gharama kubwa kwa kilo na kusababisha wanachi kushindwa kununua
Usambazaji huo ulifanywa na wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula(NFRA) katika maeneo ambayo yalionekana kuuza bidhaa hiyo kwa bei kubwa na hasa sehemu ambazo kulikuwa na upungufu wa chakula
Akiongea na Kitengo cha Mawasilioano Serikalini Kaimu Meneja wa Kanda ya NFRA Dodoma bwana Felix Ndunguru amesema lengo la zoezi hili ni Kukabiliana na upandaji wa bei za chakula katika baadhi ya halmashauri na kupunguza bei ya mahindi
Bwana Ndunguru alisema kwamba zoezi lilianza tarehe 16/5 /2017 na litaendelea mpaka mwezi wa 17 /6/2017 ambapo katika Kanda ya Dodoma Halmashauri zilizolengwa ni Manyoni, Itigi, Chamwino, Nchemba Bahi na Kondoa ambapo zilionekana bei ya nafaka kuwa juu .
Aidha katika kanda ya Dodoma Bwana Ndunguru anasema zoezi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani kabala serikali kupitia wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula ( NFRA) kusambaza mahindi kwa bei nafuu, kilo moja ya mahindi ilikuwa inauzwa katika shilingi 1300 mpaka 1500 ambapo baada ya usambazaji huo bei ya mahindi imeshukwa hadi kufikia shilingi 600 hadi 800 kwa kilo katika maeneo mengi ya mji huo
Hata hivyo Bwana Nduguru alisema zoezi la usambazaji wa chakula kwa bei nafuu ni la kitaifa kwa sababu linahusisha kanda zote zilizoko chini ya wakala wa taifa wa uhifadhi wa chakula.
Aidha Kanda ya Shinyanga inayojumuisha Mkoa wa Tabora, Mwanza, Mara na Shinyanga na Simiyu walipata mgao wa tani 4000 ambazo zilikuwa zimegawanywa katyika Halmashauri ambazo zilionekana kuwa na uhaba wa chakula
Alipohojiwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bwana Jeremia Kilembe Kaimu Meneja wa Kanda hiyo alisema kuwa tani 3600 zimeshauzwa zikabaki tani 400 ambazo nazo zinategemewa kuuzwa hivi karibu
‘Wananchi wamepokea zoezi vizuri na ndio maana tulikuwa tumepangiwa kuuza tani 4000 mpaka sasa tayari tani 3600 zimeuzwa zimebaki 400”
Hata hivyo bwana jeremia alisistiza kwamba katika maeneo ya Musoma uhitaji wa mahindi ni mkubwa sana ukilinganishwa na sehemu nyenginezo.
Naye Ramadhani Athumani Nondo Kaimu meneja Kanda ya kaskazini Arusha inayohusisha Mikoa ya Manyara,Kilimanjaro na Babati anasema mahindi yalisambazwa katika wilaya nane(8) za Babati, mbulu,Simanjiro,Mwanga ,Same,Longido,Munduli na Loliondo.
Kwa mujibu wa bwana Nondo zoezi lilifanikiwa kwakiasi kikubwa kwani mfumuko wa bei ulishapunguwa kutoka shilingi 1500 kwa kilo mwanzoni hadi kufikia shilingi 1000 baada ya kuingiza mahindi sokoni
“Bei elekezi 650 ila serikali ya wilaya nayo inapanga bei zake lakini hazizidi 800 kutegemeana na umbali kutoka kijiji hadi kijiji alisema”. Bwana Nondo.
Chanzo Tovuti ya Wizara ya Kilimo