Thursday, November 20, 2014

KUITWA KAZINI

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 21 Oktoba hadi tarehe 05 Novemba, 2014 kuwa waliofaulu usaili husika mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilishwa.

Orodha ya majina yao ni kama yanavyoonekana katika Tangazo hili. Aidha, Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa ambao walikuwa kwenye kanzidata kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana. Waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda ambao umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.

Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao. Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.

Download Here