Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Mifugo na Uvuvi anatangazia umma kuwa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za
Wakulima – Nane Nane mwaka 2017, zitaadhimishwa ngazi ya Ki-Taifa katika
Uwanja wa Maonyesho ya Kilimo wa Ngongo, Manispaa ya Lindi.
Aidha, maadhimisho ya Ki-Kanda yatafanyika katika viwanja vya maonesho ya John Mwakangale –Mbeya; Mwalimu J.K. Nyerere –Morogoro; Themi – Arusha; Nzuguni - Dodoma; na Nyahongolo – Mwanza.
Maandalizi, maonesho na sherehe za Ki-Taifa yanaratibiwa na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na uongozi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara. Maandalizi, maonesho na sherehe za Ki-Kanda yanaratibiwa na uongozi wa mikoa husika.
Vile vile, Chama cha Kilimo Tanzania (TASO) kilichokuwa kinaratibu maandalizi, maonesho na sherehe za Wakulima (Nane Nane) miaka ya nyuma kimefutiwa usajili wake mwezi Mei 2017. Hivyo kuanzia sasa utaratibu wa mandalizi, maonesho na sherehe za wakulima (Nane Nane) ni kama ulivyotolewa katika tangazo hili.
Washiriki wa maonesho ya kilimo na sherehe za Ki-Taifa wawasiliane moja kwa moja na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi au Sekretarieti za Mikoa ya Lindi na Mtwara. Pia, washiriki wa maadhimisho ya Ki-Kanda wanatakiwa kuwasiliana na Sekretarieti za Mikoa husika ili kupata maelekezo na taratibu zingine za ushiriki.
Maelezo zaidi kuhusu maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima yataendelea kutolewa kupitia:-
www.kilimo.go.tz; www
tzagriculture.blogspot.com;
www.facebook.com/tzagriculture; na
www.twitter.com/tzagriculture
WOTE MNAKARIBISHWA
Source : Wizara ya Kilimo